Get instant SMS job alerts on your phone — no app needed! Subscribe from TZS 1,000 →
JobsTanzania

Wahudumu/Wauzaji wa Vinywaji (5 Positions)

JobsTanzania

Geita Full Time Hospitality Negotiable

Posted 3 hours ago · Expires Sep 19, 2026

Job Description

Muhtasari wa Kazi

Biashara inayokua ya vinywaji (Grocery/Bar) jijini Geita inatafuta Wahudumu/Wauzaji wa Vinywaji watano (5) wenye uwezo wa kutoa huduma bora kwa wateja na kusaidia kuongeza mauzo. Tunatafuta watu wenye mwonekano nadhifu, wachangamfu, wanaopenda kuhudumia wateja na wenye uwezo wa kuwasiliana kwa lugha nzuri na ya kuvutia.

Majukumu Makuu

  • Kuuza vinywaji na kuwahudumia wateja kwa weledi.
  • Kuwakaribisha na kuwahudumia wateja kwa kauli nzuri na heshima.
  • Kuelewa mahitaji ya wateja na kupendekeza bidhaa zinazowafaa.
  • Kuhakikisha usafi wa eneo la kazi na mpangilio mzuri wa bidhaa.
  • Kusaidia kufikia malengo ya mauzo ya biashara.
  • Kudumisha mazingira mazuri ya huduma kwa wateja wakati wote.

Sifa na Mahitaji

Waombaji wanapaswa kuwa na:

  • Umri kati ya miaka 20 hadi 28.
  • Angalau miaka 1-2 ya uzoefu katika huduma kwa wateja, mauzo au kazi zinazofanana.
  • Mwonekano nadhifu, usafi wa hali ya juu na kujali mwonekano binafsi.
  • Uwezo mzuri wa kuwasiliana na kujenga mahusiano mazuri na wateja.
  • Uchamgamfu wa hali ya juu na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira yenye wateja wengi.
  • Uaminifu, nidhamu na uwajibikaji.
  • Uwezo wa kufanya kazi bila usimamizi wa karibu.

Sifa Zitakazopewa Kipaumbele

Tunapendelea waombaji wenye:

  • Ukarimu na huduma bora kwa wateja.
  • Kauli nzuri na stadi za mawasiliano.
  • Uwezo wa kuvutia na kuhudumia wateja kwa weledi.
  • Ufahamu wa uuzaji wa vinywaji au kazi za baa/grocery.
  • Kujituma katika kuongeza mauzo na kuridhisha wateja.

Maeneo Yanayopewa Kipaumbele

  • Geita
  • Mwanza
  • Shinyanga
  • Singida

Mshahara na Manufaa

  • Mshahara: TZS 150,000 kwa mwezi
  • Malazi yatatolewa na mwajiri.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Tuma maombi yako kupitia:

📞 WhatsApp/SMS: 0752 296 850

Mwisho wa Kutuma Maombi

23 Agosti 2026

Wanawake wenye sifa zinazotajwa hapo juu wanahamasishwa zaidi kutuma maombi yao.

Share this job

Share on WhatsApp

Apply for this position

Apply on Company Site

About the Company

JobsTanzania

Dar es Salaam

Similar Jobs